Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 16:58

Burundi yamfukuza mwanadiplomasia wa Rwanda


Rais wa Burundi Piere Nkurunziza, aliyevalia suti

Serikari ya Burundi ilimfukuza kwenye ardhi yake mwanadiplomasia kutoka Rwanda siku ya Jumatano .

Bwana Desire Nyaruhihira alikuwa akihudumu kama mshahuri mkuu kwenye ubalozi wa Rwanda jijini Bujumbura.

Hatua hii imechukuliwa huku uhusiano wa Burundi na Rwanda nchi hizo zinazopakana ukiwa umezorota tangu mwishoni mwa mwezi wa Aprili tangu Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza alipotangazwa na chama chake kuwa mgombea urais kwa muhula wa tatu

Ilikuwa kama uvumi kwa wiki kadhaa jijini Bujumbura kuwa mwanadiplomasia huyo amefukuzwa, lakini Jumatano waziri wa Burundi anayehusika na masuala ya kimataifa bwana Emenya Mitwe alithibitisha kuwa mwanadiplomasia huyo amefukuzwa.

Alisema mwanadiplomasia aliyekuwa akifanya kazi katika ubalozi wa Rwanda kama mshauri mkuu hatakiwi tena kukanyaga Rwanda kuanzia Jumatano.

Serikali ya Rwanda bado haijaelezea sababu za kumfukuza mwanadiplomasia huyo huku pia raia wengine wa Rwanda wanaoishi katika mkoa wa Kayanza walifuzwa mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba.

XS
SM
MD
LG