Mazungumzo kati ya chama tawala nchini burundi- CNDD –FDD, upinzzani , mashirika ya kiraia pamoja na wadau wowote wa kisiasa chini ya rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni yanaendelea.
Mwandishi wetu Haidalah Hakizimana anaripoti kwamba suala lililotanda katika mjadala huu ikiwa leo ni siku ya tatu ni usalama , ambapo mambo makuu manne yalitakiwa kujadiliwa ikiwemo muhula wa tatu wa uongozi, kalenda ya uchaguzi kubadilishwa na serikali ya ushirikiano wa madaraka kufikiriwa.
Hakuna maadhimio rasmi yaliyojitokeza hadi sasa ingawa bado upande wa serikali unasisitiza kwamba lazima uchaguzi wa urais ufanyike tarehe 21 mwezi huu huku wapinzani wakiendelea kusuisa na kutaka uahirishwe.
Kuna wagombea watatu wa urais kutoka upande wa upinzani walioondoa majina yao katika kinyang’anyiro hicho.
Hali kwa ujumla ni shwari ingawa watu hawana mwamko wa uchaguzi huo wala shauku katika kampeni za uchaguzi. Baadhi ya watu wameanza kukimbia nchi kutokana na utata ndani ya uchaguzi huo .