Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:22

Nkurunzinza atangazwa kiongozi wa maisha wa chama cha CNDD/FDD


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika ikulu ya raisBujumbura, Burundi. Juni, 2017.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika ikulu ya raisBujumbura, Burundi. Juni, 2017.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametangazwa na chama chake kuwa ni kiongozi wa kudumu na mahiri asiyelinganishwa na yoyote.

‘’Ninatumia fursa hii kutangazia waliojariwa kufika hapa kuwa kamati kuu ya chama chetu cha CNDD FDD imechukuwa hatua kuwa mheshimiwa rais wa nchi yetu Pierre Nkurunzinza ndiye wa kwanza, ni kiongozi mahiri kwetu, ni mzazi anayetushahuri, asiyelinganishwa na mtu yoyote.Ninaomba wafuasi wa chama chetu kuheshimisha hatua hii’’ alisema Evariste Ndayishimiye katibu mkuu wa chama tawala Burundi cha CNDD FDD siku ya Jumamosi akiwa tarafani Mwumba katika mkoa wa nyumbani kwa rais Nkurunziza.

Ilikuwa katika sherehe za kukamilisha kile kilichofahamika kama mashindano ya kitamaduni yaliyoandaliwa na chama cha CNDD FDD.Lakini katibu mkuu wa chama cha CNDD FDD hakufafanua zaidi maneno hayo na athari yake kwa utawala wa nchi.

XS
SM
MD
LG