Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:41

Marais wa Afrika wakamilisha ziara yao Burundi


Jacob Zuma, Rais wa Afrika kusini akiongoza ujumbe wa AU huko Burundi aweka shada la mauwa kwenye kaburi la rais wa kwanza wa kidemokrasia Melchior Ndadaye, Bujumbura Februari 25 2016. (AP Photo)
Jacob Zuma, Rais wa Afrika kusini akiongoza ujumbe wa AU huko Burundi aweka shada la mauwa kwenye kaburi la rais wa kwanza wa kidemokrasia Melchior Ndadaye, Bujumbura Februari 25 2016. (AP Photo)

Marais wanne pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia, ambao wamekuwa ziarani nchini Burundi kujaribu kuishawishi serikali ya nchi hiyo na upinzani kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao, walimaliza ziara hiyo Ijumaa jioni.

Hata hivyo, viongozi hao hawakutoa taarifa yoyote kuhusu kile walichokubaliana na pande husika.

Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma aliongoza ujumbe huo wakati marais hao wakikutana faraghani na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika ikulu yake mjini Bujumbura.

Zuma amewaambia waandishi wa habari kuwa wamekubaliana mengi na wadau waliozungumza wakati wa ziara hiyo iliyoanza jana Alhamisi.

Hata hivyo hakuyataja waliyoyajadili na amekataa kujibu maswali ya wandishi wa habari akisema kuwa maswali yatajibiwa hapo kesho baada ya kutoa tangazo la yale waliokubaliana.

Marais hao ni pamoja na kiongozi wa Mauritania Muhamed Ould abdelaziz, wa Senegal Macks Sall, wa afrika ya kusini Jacob zuma, Rais wa Gabon Ali Bongo pamoja wa waziri mkuu wa Ethipitia Haile Mariam desalein.

XS
SM
MD
LG