Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:04

Rais Nkurunziza afuta mawaziri watatu.


Waandamanaji watawanywa Bujumbura.
Waandamanaji watawanywa Bujumbura.

Rais wa Burundi amewafuta kazi mawaziri watatu huku maandamano yakianza tena baada ya jaribio la kupindua serikali kufeli wiki iliopita. Msemaji wa rais amaeiyambia idhaa ya VOA ya Afrika ya kati Jumatatu kuwa rais Pierre Nkurunziza amewatimua mawaziri wa ulinzi, uhusiano wa kigeni na waziri wa biashara.

Wanajeshi Jumatatu walifyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamefunga barabara wakipinga uamuzi wa Bw Nkurunziza wa kuwania urais kwa muhula wa tatu. Shughuli za biashara zilifungwa katika maeneo ya Nyakabiga, Musaga na Mutakura mjini Bujumbura lakini hali ilikuwa tulivu kwenye maeneo yanayomuunga mkono rais.

Jumapili, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alizungumza na mwenzake wa Burundi kwa njia ya simu akimsihi kuahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwezi ujao. Wengi wa viongozi walioongoza jaribio la kupindua serikali wamekamatwa lakini Generali Godefroid Niyombare aliyetangaza mapinduzi hayo kwenye radio angali anasakwa.

XS
SM
MD
LG