Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 10:30

Ban Ki-moon aitaka AU haraka kusitisha ghasia Burundi


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia katika kikao cha 26 cha Umoja wa Afrika nchini Ethiopia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia katika kikao cha 26 cha Umoja wa Afrika nchini Ethiopia.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-Moon amesema Jumapili kwamba viongozi wa Afrika hawawezi kusubiri zaidi kuzungumzia ghasia nchini Burundi, akisema kuwa muda unapita huku watu zaidi wakiuawa huko.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika nchini Ethiopia, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameiita hali ya taifa hilo ni suala heshima na haki za binadamu.

“ Ndiyo maana ni suala la uharaka ambalo mimi nawasihi viongozi wa Afrika kuchukua hatua kwa sauti moja, na hasa kumsihi rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza na serikali yake kusikiliza kwa makini sana na kujihusisha katika majadiliano ya wote", amesema Ban.

Jumamosi, Ban aliuambia mkutano wa viongozi kwamba walinzi wa amani ni muhimu nchini Burundi ambapo serikali imeonya kwamba kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Afrika kitaonekana kama ni uvamizi katika nchi.

AU inafikiria kupeleka kikosi cha walinzi wa amani 5,000 kutokomeza ghasia za kisiasa ambazo zilizuka mwaka jana wakati rais Nkurunzia alipotangaza kuwa atawania awamu ya tatu ya uongozi. Wapinzani wake wanasema hilo lilikuwa kinyume cha katiba.

Tangu wakati huo, takwimu za kimataifa zinaonyesha zaidi ya watu 400 wameuawa nchini Burundi, huku ushahidi mpya ukibaini kuna makaburi ya jumla karibu na mji mkuu.

Theluthi mbili ya mataifa wanachama 54 wa Umoja wa Afrika wanahitajika kuidhinisha upelekaji wa kikosi cha ulinzi wa amani nchini Burundi.

XS
SM
MD
LG