Hii ilikuwa ni baada ya dakika 120 kumalizika bila mshindi wakiwa wamefungana bao moja kwa moja .
Alikuwa ni mshambuliaji wa Burkinafaso Bertrand Traore na nahodha wa timu hiyo anayechezea timu ya ligi ya Uingereza Aston Villa aliyepachika bao kunako dakika ya 28 baada ya kupokea pasi kutoka kwa mchezaji mdogo kuliko wote katika michuano hiyo Dango Outtara mwenye umri wa miaka 19.
Traore alisahihisha makosa yake baada ya kukosa penati kunako dakika ya 18 ya mchezo huo ambapo shuti lake liligonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani.
Mchezo ulikuwa ni mkali na maamuzi ya kutatanisha ikiwa ni pamoja na kutolewa jumla ya kadi 13 za njano na moja nyekundu aliyopewa mchezaji wa Gabon Sidney Obissa katika dakika ya 67.
Na katika dakika za majeruhi itabidi Burkina Faso wajilaumu wenyewe baada ya kuwapa zawadi Gabon baada ya mchezaji Adama Guira kujifunga goli akijaribu kuokoa mpira wa kichwa kwenye kona golini kwake na kusababisha mchezo huo kuisha kwa sare ya bao 1-1 na kwenda dakika 30 za nyongeza.
Na baada ya dakika 120 ndipo timu hizo zikaingia katika hatua ya penati.