Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 15, 2024 Local time: 05:34

Burkina Faso yasimamisha vyombo vya habari vya Magharibi na Afrika kutokana na kutangaza ripoti ya Shirika la HRW


Mwanajeshi wa Burkina Faso akipita karibu na gari la kijeshi la kinajeshi la Ufaransa katika sehemu ya msafara wa wanajeshi wa Ufaransa unaoelekea Niger, na kusimamishwa na waandamanaji huko Kaya, Burkina Faso, Jumamosi Novemba 20, 2021.
Mwanajeshi wa Burkina Faso akipita karibu na gari la kijeshi la kinajeshi la Ufaransa katika sehemu ya msafara wa wanajeshi wa Ufaransa unaoelekea Niger, na kusimamishwa na waandamanaji huko Kaya, Burkina Faso, Jumamosi Novemba 20, 2021.

Burkina Faso imevisimamisha vyombo vya habari vingi vya Magharibi na Afrika kutokana na kutangaza ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu (HRW) inayolishutumu jeshi hilo kwa mauaji ya kiholela, mamlaka yake ya mawasiliano ilisema Jumapili.

Hatua hiyo inafuatia kusimamishwa pia kwa shirika la BBC na Sauti ya Amerika inayofadhiliwa na serikalini ya Marekani kwa kuripoti uchunguzi wa Human Rights Watch ambao ulidai kuwa jeshi la Burkina faso liliwanyonga wanakijiji wapatao 223 mwezi Februari kama sehemu ya kampeni yake dhidi ya raia wanaotuhumiwa kushirikiana na wanamgambo wa kijihadi.

Baraza la mawasiliano la nchi hiyo ya Afrika Magharibi linaloongozwa na jeshi lilisema matangazo ya televisheni ya Ufaransa TV5 Monde yatasitishwa kwa wiki mbili, huku tovuti yake kuzuiwa.

Tovuti za shirika la utangazaji la Ujerumani Deutsche Welle, magazeti ya Ufaransa Le Monde na Ouest-France, gazeti la Uingereza la The Guardian, na mashirika ya Afrika ya APA na Ecofin pia yamezuiliwa hadi taarifa zaidi, ilisema.

Reuters haikuweza kufikia vikundi vya habari mara moja kwa maoni.

Siku ya Jumamosi, msemaji wa serikali ya Burkinafaso Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo alikanusha madai ya HRW kama tuhuma “zisisizo na msingi” na akakanusha kuwa mamlaka hazikuwa tayari kuchunguza madai ya ukatili.

Mauaji hayo yamepelelkea kufunguliwa kwa uchunguzi wa mahakama, Ouedraogo alisema, akinukuu taarifa ya Machi mosi ya mwendesha mashtaka wa eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG