Sankara, mwanamapinduzi ambaye alikua anafuata siasa za ki Marxist aliyekua anaitwa mara nyingi “ Che Guevara wa Afrika” aliuwawa wakati wa mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na rafiki yake wa zamani, Compaore.
Compaore aliiongoza Burkina Faso kwa kipindi cha miaka 27 kabla ya kuondolewa madarakani mwaka 2014 na kukimbilia nchini Ivory Coast, ambako inaaminika bado anaishi huko. Awali, alikanusha kuhusika katika kifo cha Sankara.
Jopo la kijeshi lilimfungulia mashtaka Compaore anayeshutumiwa kwa kula njama katika mauaji hayo, kuhatarisha usalama wa taifa, waraka wa mahakama umeonyesha.
-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC.