Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 20:37

Bunge la Zimbabwe lapitisha sheria yenye utata inayohamasisha uzalendo


Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoa hotuba kuhusu hali ya taifa kwenye bunge mjini Harare, Novemba 23, 2022.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoa hotuba kuhusu hali ya taifa kwenye bunge mjini Harare, Novemba 23, 2022.

Mswaada huo ambao uliidhinishwa na bunge Jumatano jioni, unaharamisha vitendo vinavyohujumu “uhuru na maslahi ya taifa” ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Wanaokiuka sheria hiyo wanakabiliwa hadi kifungo cha miaka 20 jela.

“Uhuru wa kujieleza umekufa,” mwandishi wa habari mashuhuri na mwanaharakati Hopewell Chin’ono ameandika kwenye Twitter, akiongeza kuwa ilikuwa “siku mbaya sana kwa Zimbabwe.”

Sheria hiyo ilipitishwa saa chache baada ya serikali kuondoa hali ya sintofahamu kwa miezi kadhaa, na kutangaza kwamba uchaguzi wa kitaifa utafanyika tarehe 23 Agosti.

Joseph Chinotimba, mbunge kutoka chama tawala cha ZANU-PF aliliambia bunge kwamba sheria hiyo mpya inalenga kuhamasisha Wazimbabwe kuwa “wazalendo.”

Lakini wapinzani wamesema inapiga marufuku ukosoaji wa serikali wakati ambapo makundi ya haki za binadamu na vyama vya upinzani tayari wamelalamika juu ya ukandamazaji.

Forum

XS
SM
MD
LG