Baadhi ya wabunge na wanaharakati nchini Uganda wanasema upigaji kura kuhusu sheria yenye utatanishi dhidi ya ushoga umeahirishwa.
Spika wa bunge, Edward Ssekandi ameahirisha bunge Ijumaa akisema hakuna muda wa kutosha kuanza mjadala kuhusu mswaada huo.
Kikao cha sasa cha bunge kinamaliza shughuli zake jumatano. Mswaada unataka adhabu ya kifo iwe ni lazima kwa baadhi ya vitendo vya ushoga na imeshutumiwa vikali na Marekani na makundi mbali mbali haki za binadamu.
Rais wa Marekani Barack Obama ameelezea kuwa itasababisha chuki. Mwandishi wa mswaada huo David Bahati alisema mapema wiki hii kwamba mswaada uliorekebishwa hautakuwa na kifungu cha adhabu ya kifo.
Kundi la kutetea haki za binadamu la Avaaz limesema wabunge kukataa kuchukua hatua zozote ni ushindi kwa waganda wote.