Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:07

Bunge la Pakistan kumchagua waziri mkuu mpya baada ya kura ya kutokuwa na imani na Imran Khan.


Wafuasi wa chama cha waziri mkuu wa Pakistan aliyefutwa kazi Imran Khan, wakipeperusha bendera za chama cha PTI, wakihudhuria mkutano wa kumuunga mkono mjini Karachi April 10, 2022. Picha ya AFP
Wafuasi wa chama cha waziri mkuu wa Pakistan aliyefutwa kazi Imran Khan, wakipeperusha bendera za chama cha PTI, wakihudhuria mkutano wa kumuunga mkono mjini Karachi April 10, 2022. Picha ya AFP

Pakistan leo Jumatatu inapiga kura kumchagua kiongozi wa upinzani Shehbaz Sharif kama waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, siku moja baada ya bunge la taifa kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu wa sasa Imran Khan, na hivyo kumaliza uongozi wa miaka minne wa serikali yake ya ushirika.

Bunge la taifa lenye wabunge 342 mapema Jumapili lilipiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Imran Khan, huku wabunge 174 wa muungano wa upinzani wakiunga mkono, ni mara mbili zaidi ya idadi iliyokuwa inahitajika kumshinikiza nyota huyo wa zamani wa mchezo wa kriketi kuondoka madarakani.

Sharif aliongoza mchakato wa upinzani katika juhudi za kumuondoa madarakani Khan, na baadaye aliwasilisha uteuzi wake kwa bunge ili achaguliwe kama waziri mkuu, uchaguzi ambao mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 anatarijwa kuushinda.

Khan ni waziri mkuu wa kwanza nchini Pakistan kuondolewa kupitia kura ya kutokuwa na imani naye, lakini hakuna waziri mkuu aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia aliyehudumu muhula kamili wa miaka mitano tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka wa 1947.

XS
SM
MD
LG