Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:34

Waripablikan waahirisha vikao vya bunge


Wajumbe kutoka chama cha Repablikan mapema leo wameahirisha vikao hadi Julai 5 baada ya wademokrat kugomea mjadala ndani ya Bunge kwa zaidi ya saa 16 wakiitisha kura kupigwa kuhusiana na umiliki wa bunduki.

Ulikuwa usiku wenye vituko ndani ya Bunge hilo maarufu Capitol Hill ambapo wajumbe warepablikan walirudi ndani kupiga kura huku wenzao wa chama cha Democrat wakisusia na kusema ‘No Bill, No Break' wakati wakiendelea kumfokea Spika wa Bunge Paul Ryan.

Mwanaharakati mashuhuri wa kutetea haki za raiya, John Lewis, kutoka jimbo la Georgia amepongeza wajumbe wa chama cha Democrat kwa kuchukua hatua ya kutathmini sheria za umiliki wa bunduki hasa baada ya mauwaji yaliotokea Orlando, Florida wiki moja iliopita huku akiwahimiza wenzao wa chama cha Repablikan kupitisha mswada huo.

​
XS
SM
MD
LG