Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:09

Warepublikan wapiga kura kukataa mapendekezo ya kudhibiti silaha.


Siku nane baada ya mauaji mabaya kuliko yote katika historia ya Marekani bunge la Marekani limepiga kura kukataa mfululizo wa mapendekezo kuzuia wale walio na haki ya kununua bunduki na kuongeza uchunguzi kwa wanunuzi wa bunduki.

Jumatatu usiku warepublikan walizuia mapendekezo ya muda mrefu ya wademokrat na mpango mpya baada ya mshambuliaji aliyevutiwa na kundi la Islamic State Omar Mateen kuuuwa watu 49 na kujeruhi 53 wengine baada ya wiki moja tu huko Orlando Florida.

Hatua moja itawazuia wale wanaochunguzwa na serikali kuu ya ugaidi ikiwa ni pamoja wale waliozuiwa kupanda ndege , kununua silaha. Nyingine ni kuongeza uchunguzi wa historia za watu kwa lazima kwa manunuzi ya silaha ikiwa ni pamoja na maonyesho ya silaha na mauzo kwenye mitandao.

Mapendekezo yote yameshindwa kupata uungaji mkono wa tatu ya tano inayohitajika ili kuweza kupitishwa kama marekebisho kwenye muswaada unaosubiri kupitishwa kuwa sheria.

XS
SM
MD
LG