Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:57

Bunge la Kenya limehoji hatua ya serikali kutuma wanajeshi DRC


Wanajeshi wa Kenya KDF baada ya kupokea bendera kutoka kwa rais Dkt. William Ruto, tayari kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na makundi ya waasi Nov 2, 2022
Wanajeshi wa Kenya KDF baada ya kupokea bendera kutoka kwa rais Dkt. William Ruto, tayari kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na makundi ya waasi Nov 2, 2022

Wabunge wa Kenya wanahoji hatua ya serikali ya nchi hiyo kutuma wanajeshi wake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na makundi ya waasi, bila idhini ya bunge.

Katika kikao cha bunge jana Alhamisi, wabunge walisema kwamba serikali imekiuka sheria kwa kutuma barua kwa bunge kuidhinisha hatua ya kupeleka wanajeshi nchini DRC, wakati tayari rais William Ruto alikuwa amehudhuria hafla ya wanajeshi hao kwenda nchini humo.

Mbunge wa Tiaty William Kamket, alilieleza bunge kwamba waziri wa ulinzi Adan Duale, aliwasilisha barua ya serikali kwa bunge Jumatano, kuliarifu nia ya serikali ya Kenya kutuma kikosi cha kulinda amani nchini DRC, na kudai kwamba sheria imekiukwa, na kwamba bunge lingepewa taarifa kwanza, kujadiliwa, kabla ya rais Ruto kuweka rasmi kwamba wanajeshi wa Kenya wanakwenda DRC.

Sehemu ya 8 ya ibara ya 240 ya katiba ya Kenya inataka bunge kuidhinisha hatua yoyote ya wanajeshi wa Kenya kuingia nchi nyingine kwa ajili ya kulinda amani.

Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula amesema kwamba barua ya waziri wa ulinzi ilifika bungeni Jumatano asubuhi, na baadaye adhuhuri, rais Ruto kahudhuria hafla ya kuwaaga wanajeshi wa Kenya kwenda DRC.

XS
SM
MD
LG