Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 13, 2025 Local time: 10:40

Bunge la Iran lapendekeza adhabu kali kwa wahusika wa ukatili dhidi ya wanawake


Rais wa Iran Ebrahim Raisi akihutubia wabunge, Januari 22, 2023.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi akihutubia wabunge, Januari 22, 2023.

Bunge la Iran limeidhinisha mapendekezo ya kutoa adhabu kali kwa wahusika wa ukatili dhidi ya wanawake, mapendekezo ambayo yanaweza kupitishwa na kuwa sheria ndani ya miezi michache, shirika la habari la serikali limeripoti.

Yakianzishwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, majadaliano bungeni yalipelekea kupitishwa siku ya Jumapili kwa kanuni za jumla za mswada uliotajwa kuwa “wa kuzuia madhara kwa wanawake na kuboresha usalama wao dhidi ya tabia mbaya, IRNA imeripoti.

Mswada huo ambao unaweza kufanyiwa marekebisho, unaweza kusainiwa rasmi na kuwa sheria katika miezi ijayo.

Mchakato huo unajiri takriban miezi saba baada ya maandamano ya nchi nzima yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini kilichotokea mwezi Septemba akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Mwanamke huyo wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22 alikamatwa kwa madai ya kukaidi sheria kali ya mavazi kwa wanawake.

​
XS
SM
MD
LG