Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 06:41

Bunge la EU lairuhusu Ukraine kuwania uanachama wa Umoja wa Ulaya


Wabunge wa Umoja wa Ulaya na waakilishi wa Ukraine wakishika bendera refu ya Ukraine nje ya bunge la EU, kabla ya upigaji kura wa kuipa Ukraine hadhi ya kuwania uanachama wa EU, June 23, 2022. Picha ya Reuters
Wabunge wa Umoja wa Ulaya na waakilishi wa Ukraine wakishika bendera refu ya Ukraine nje ya bunge la EU, kabla ya upigaji kura wa kuipa Ukraine hadhi ya kuwania uanachama wa EU, June 23, 2022. Picha ya Reuters

Bunge la Umoja wa Ulaya Alhamisi limepiga kura kwa wingi kuipa hadhi Ukraine ya kuwania uanachama wa Umoja huo, hatua muhimu ambayo inaifanya Ukraine kukaribia kujiunga na nchi za magharibi ambazo zimeipa vifaa vingi vya kijeshi ili kuisadia kupambana na uvamizi wa miezi minne wa Russia.

Wabunge 529 ndio wamepitisha hadhi hiyo, 45 wakaipinga, na 14 wakijizuia kupiga kura. Bunge hilo la Umoja wa Ulaya limeidhinisha pia uwaniaji wa Georgia na Moldova wa kuwa wanachama.

Spika wa Bunge la Ukraine Ruslan Stefanchuk aliwashukuru wabunge wa Umoja wa Ulaya kwa uungaji wao mkono kwa Ukraine katika ujumbe kwenye Facebook, akisema, “Ukraine ni nchi mwanachama wa EU. Na tunapigania haki hii sio tu kwenye uwanja wa vita lakini pia katika nyanja ya kisheria.”

Ili nchi hizo tatu zijiunge rasmi na jumuia hiyo ya nchi wanachama 27, zitatakiwa kufanya mageuzi kadhaa ya kisiasa na kiuchumi.

Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema Ukraine “ imekwisha tekeleza karibu asilimia 70 ya sheria, kanuni na vigezo vya EU.”

Amesema hata hivyo, mengi yanahitajika kufanyika kwenye sekta za utawala wa sheria, kupambana na ufisadi na haki za kimsingi.”

XS
SM
MD
LG