Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 19, 2025 Local time: 07:17

Bunge la Ethiopia limeiondoa TPLF kama kundi la kigaidi


Wabunge ndani ya bunge la Ethiopia
Wabunge ndani ya bunge la Ethiopia

Ujumbe wa bunge  kwenye ukurasa wa Facebook unaeleza uamuzi wa kuondoa TPLF kama kundi la kigaidi umepita kwa kura nyingi,"   Ujumbe umesema hatua hiyo itaimarisha makubaliano ya amani ya Novemba 2022 kati ya TPLF na serikali kuu

Bunge la Ethiopia siku ya Jumatano lilikiondoa chama cha waasi cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) katika orodha rasmi ya makundi ya kigaidi hatua muhimu katika mchakato wa amani kufuatia mzozo wa miaka miwili huko kaskazini mwa nchi hiyo.

Ujumbe wa bunge kwenye ukurasa wa facebook unaeleza kwamba, uamuzi wa kuondoa TPLF kama kundi la kigaidi umepita kwa kura nyingi," Ujumbe umesema hatua hiyo itaimarisha makubaliano ya amani ya Novemba 2022 kati ya TPLF na serikali kuu Ilielezwa wakati wa majadiliano ya rasimu ya uamuzi kwamba kuondoa jina la kigaidi la TPLF ni muhimu kuzingatia makubaliano ya amani yaliyofanyika kati ya serikali kuu na TPLF"

TPLF ambayo wakati mmoja ilikua chama kikuu cha kisiasa nchini Ethiopia, iliteuliwa rasmi kuwa kundi la kigaidi hapo Mei 2021 miezi sita baada ya vita kuzuka.

XS
SM
MD
LG