Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:47

Bunge la Afrika Kusini lateua jopo huru kubaini iwapo Rais Ramaphosa anapaswa kufunguliwa mashtaka


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza katika ufunguzi wa kiwanda cha Sandvik Khomanani.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza katika ufunguzi wa kiwanda cha Sandvik Khomanani.

Bunge la Afrika Kusini limeteua jopo huru kubaini iwapo Rais Cyril Ramaphosa anapaswa kufunguliwa mashtaka bungeni kwa madai ya kuficha wizi katika nyumba yake ya kifahari ya shambani.

Spika wa bunge Nosiviwe Mapisa-Nqakula alitangaza kuteuliwa kwa jopo hilo katika taarifa iliyotolewa Jumatano usiku.

Jopo hilo linajumuisha jaji mkuu wa zamani Sandile Ngcobo, jaji mashuhuri wa zamani wa mahakama kuu na muhadhiri wa chuo kikuu.

Kumuondoa madarakani rais kunahitaji theluthi mbili ya kura katika bunge la taifa, lakini

chama cha Ramaphosa cha African National Congress (ANC) kina zaidi ya theluthi mbili ya viti bungeni.

Chama kidogo cha upinzani, the African Transformation Movement (ATM), kiliwasilisha hoja iliyopelekea kuundwa kwa jopo hilo.

Kashfa inayomuhusu Ramaphosa ilizuka mwezi Juni baada ya mkuu wa zamani wa idara ya taifa ya ujasusi, Arthur Fraser, kuwasilisha malalamiko kwa polisi.

Alidai kwamba majambazi walivamia shamba la rais kaskazini mashariki mwa nchi, ambapo waliiba pesa taslimu dola milioni 4 zilozofichwa kwenye fanicha.

XS
SM
MD
LG