Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 01:04

Brazil: Wafuasi 1,000 wa Rais wa zamani Bolsonaro wahojiwa na polisi


Wafuasi wa Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro wakisimama kwenye paa la jengo la Bunge baada ya kulivamia mjini Brazilia, Januari 8, 2023

Polisi wa Brazil Jumanne waliwahoji karibu wafuasi 1,000 wa Rais wa zamani mwenye siasa kali za mrengo wa kulia Jair Bolsonaro wanaoziuiliwa kwenye ukumbi wa mazoezi katika mji mkuu, Brasilia.

Wanachunguza vurugu dhidi ya serikali mwishoni mwa juma ambazo ziliharibu vibaya majengo ya umma katika maandamano dhidi ya Rais mpya Luiz Inacio Lula da Silva.

Wafungwa hao walikuwa wamekaa katika kambi moja ya mjini Brazilia iliyobomolewa na wanajeshi Jumatatu, siku moja baada ya mamia ya waandamanaji kuondoka kwenye kambi hiyo na kuvamia majengo ya Bunge la Brazil, Mahakama ya Juu na Ikulu.

Waandamanaji walitoa wito wa mapinduzi ya kijeshi ili kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Oktoba ambapo Lula wa mrengo wa kushoto alimshinda kwa kura kidogo Bolsonaro.

Jaji wa Mahakama ya juu Alexandre de Moraes aliapa katika hotuba kupambana na “magaidi”.

Takriban waandamanaji 200 walikamatwa na kuzuiliwa gerezani kwa kuhusika kwao katika uvamizi wa Jumapili.

“Demokrasia itashinda na taasisi za Brazil hazitakuwa dhaifu,” Moraes alisema wakati wa kuapishwa kwa mkuu mpya wa polisi wa serikali kuu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG