Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 19:18

Brazil yajiweka sawa kundi E


Neymar wa Brazil amtoka mlinzi wa Costa Rica, Juni 22, 2018

Mchezaji nyota wa Brazil Neymar alitokwa na machozi ya furaha baada ya kipyenga cha mwisho kulia huku timu yake ikiwa imepata ushindi mgumu wa 2-0 dhidi ya Costa Rica katika mechi ya Kundi E.

Neymar alipachika bao la pili katika dakika za ziada baada ya mwenzake Philippe Coutinho kuingiza bao la kwanza la Brazil katika dakika ya 91, bao lililotuliza nyoyo za mashabiki wa Brazil ambao walikua na hofu kubwa ya kuona timu yao ikikwama kama ilivyokwamishwa Argentina ya Lionel Messi baada ya kuchapwa mabao 3 kwa nunge na timu ya Croatia katika mechi ya Kundi D Alhamisi.

Hilo lilikuwa bao la kwanza kwa Neymar katika mechi mbili za mashindano hayo. Kwa ushindi huo Brazil inaongoza kundi E ikiwa na pointi nne ikifuatiwa na Serbia yenye pointi tatu. Timu hizo mbili zitakutana katika mechi yao ya mwisho na kuamua timu zitakazoingia raundi ya michuano kutoka kundi hilo.

Costa Rica tayari wamefunga virago baada ya kushindwa mechi zake mbili za kwanza. Serbia waweza kujipatia tikiti ya kuvuka mzunguko wa kwanza endapo wataishinda Uswisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG