Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 13:37

Bozize akimbilia Cameroon


Francois Bozize, rais aliyetimuliwa madarakani Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais Francois Bozize apewa hifadhi Cameroon baada ya waasi kumtimua madarakani.

Maafisa wa Cameroon wanasema rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize amepata hifadhi nchini humo baada ya kuikimbia nchi yake wakati waasi walipochukua udhibiti wa mji mkuu.

Wakati huo, huo Umoja wa Afrika umetangaza kuwa unaifukuza Jamhuri ya Afrika ya Kati kama mwanachama wake.

Jumatatu Michael Djotodia kiongozi wa kundi la waasi Seleka alisema anachukua madaraka kama rais. Afrika Kusini imesema wanajeshi wake 13 waliuawa na wengine 27 wakajeruhiwa katika mapigano na waasi hao.

Mwanajeshi mmoja hajulikani alipo baada ya mapigano hayo kuzuka Jumamosi katika mji mkuu wa Bangui. Rais Jacob Zuma amesema vifo vya wanajeshi wake haviwezi kuepusha nchi yake kufanya kazi kuzuia kupinduliwa kwa serikali iliyochaguliwa.
XS
SM
MD
LG