Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:51

Katibu Mkuu wa zamani wa UN afariki


Boutros Boutros-Ghali
Boutros Boutros-Ghali

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Boutros Boutros-Ghali amefariki dunia, rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ametangaza Jumanne.

Boutros-Ghali alikuwa katibu mkuu wa sita wa Umoja wa Mataifa. Mwanasiasa na mwanadiplomasia huyo kutoka Misri alihudumu katika kipindi cha miaka ya 1992 mpaka1996. Boutros-Ghali ambaye alilazwa katika hospitali moja mjini Cairo, Misri wiki iliyopita na alikuwa na miaka 93.

Wakati wa uongozi wake dunia ilipitia maswala kadha magumu ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Rwanda, Angola na kuvunjika kwa taifa la zamani la Yugoslavia.

Alijaribu kupata awamu ya pili ya uongozi lakini Marekani ilitumia kura ya veto kupinga kuendelea kwake kama katibu mkuu. Wakati huo Marekani ilimshutumu Boutros-Ghali kwa kushindwa kupunguza bajeti ya Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG