Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:09

Boti yazama Kenya


Waokoaji wa kujitolea wakitafuta miili huko Lamu. (AP Photo)
Waokoaji wa kujitolea wakitafuta miili huko Lamu. (AP Photo)

Maafisa wanaendelea kutafuta walionusurika , huku 23 wakiripotiwa wameogelea nchi kavu.

Maafisa wanasema boti moja imezama kwenye kisiwa kimoja cha utalii karibu mpaka wa Somalia na kuuwa watu wapatao saba.

Maafisa wanaendelea kutafuta walionusurika Jumatatu huku dazeni ya watu wakiwa wamepotea baada ya boti hiyo kuzama Jumapili usiku ilipokuwa ikisafiri kutoka kisiwa cha Lamu kuelekea kwenye upande mwingine wa nchi kavu wa Kenya.

Idara ya Msalaba mwekundu inasema watu 25 wameokolewa , wakati 23 wengine waliweza kuogelea kuelekea ufukweni.

Watu wengi husafiri kutoka Lamu kuelekea Mombasa wakati wa sikukuu hizi na maafisa wa Polisi wameonya abiria wakipanda boti hizo wawe makini na waangalifu .

XS
SM
MD
LG