Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 06, 2025 Local time: 16:29

Jair Bolsonaro ndie Rais wa Brazil


Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro
Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro

Katika hotuba yake baada ya kula kiapo Bolsonaro ambaye ni kapteni wa zamani wa jeshi aliahidi kupunguza sheria za bunduki kuwaruhusu raia wema kumiliki silaha, na kuwaandaa watoto kwa ajili ya soko la ajira na sio uanamgambo wa kisiasa

Mwanasiasa wa mrengo wa kulia Jair Bolsonaro ameapishwa kama Rais wa Brazil akitoa ahadi ya kupambana na rushwa, uhalifu na uchumi ulioanguka.

Kapteni wa zamani wa jeshi ambaye amekuwa akiitwa Donald Trump wa Brazil, aliapishwa kushika madaraka siku ya Jumanne huko Brasilia. Rais wa Marekani, Donald Trump alimpongeza Bolsonaro kupitia Twitter akimueleza “Marekani ipo pamoja nawe. Rais huyo wa Brazil alijibu pia kwenye Twitter “chini ya ulinzi wa mungu, tutaleta mafanikio na maendeleo kwa watu wetu.

Jair Bolsonaro
Jair Bolsonaro

Bolsonaro ni kiongozi wa karibuni katika mfululizo wa viongozi wa mrengo wa kulia duniani kote ambaye ameingia madarakani huku akiwa dhidi ya wakuu wa chama.

Katika hotuba yake baada ya kula kiapo Bolsonaro aliahidi kupunguza sheria za bunduki kuwaruhusu raia wema kumiliki silaha, akiongeza kinga kwa vikosi vya usalama ambavyo vinatumia silaha nzito na kuwaandaa watoto kwa ajili ya soko la ajira na sio uanamgambo wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG