Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 03:28

Bolivia yatangaza kuvunja uhusiano wake na Israel kufuatia shambulizi la Gaza


Rais wa Bolivia Luis Arce akitoa hotuba kwa taifa. Picha ya January 22, 2023.
Rais wa Bolivia Luis Arce akitoa hotuba kwa taifa. Picha ya January 22, 2023.

Bolivia Jumanne imesema kwamba imevunja uhusiano wake na Israel kutokana na shambulizi  dhidi ya Ukanda wa Gaza, wakati mataifa jirani ya Colombia na Chile yakiwaita mabalozi wake kutoka taifa hilo la mashariki ya kati kwa mashauriano.

Mataifa hayo matatu ya Amerika kusini yamekemea mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, huku pia yakilalamikia vifo vya wananchi wa Palestina kwenye vita hivyo. Tangazo la Bolivia limetolewa na waziri wa mambo ya nje Freddy Mamani wakati akizungumza na wanahabari.

Mataifa yote matatu yameomba sitisho la mapigano, wakati Bolivia na Chile wakiomba kuruhusiwa kwa upelekaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza, huku Israel ikituhumiwa kwa kukiuka sheria za kimataifa. Rais wa Colombia Gustavo Petro ametaka mashambulizi hayo kuwa mauaji dhidi ya wa Palestina, kupitia ujumbe aliouweka kwenye mtandao wa X uliokuwa ukijuikana kama Twitter.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel amesema kwamba uamuzi wa Bolivia ni sawa na kuunga mkono ugaidi. Mataifa mengine ya Latin Amerika kama vile Mexico na Brazil pia yametoa wito wa kusitishwa mapigano.

Forum

XS
SM
MD
LG