Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:35

Boko Haram ladai kuhusika katika mashambulizi Nigeria


Watu wakiwa wamesimama nje ya kanisa baada ya mlipuko kaskazini-mashariki mwa Nigeria
Watu wakiwa wamesimama nje ya kanisa baada ya mlipuko kaskazini-mashariki mwa Nigeria

Shambulizi la kwanza lilitokea katika kanisa la kikatoliki katika mji wa Madalla, karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Abuja

Kundi la Boko Haram nchini Nigeria limedai kuhusika katika mashambulizi ya siku ya Krismas katika makanisa nchini Nigeria ambapo jumla ya watu 25 waliuawa.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika kanisa la kikatoliki wakati wa misa ya Krismas katika mji wa Madalla uliopo karibu na Abuja, mji mkuu wa Nigeria, na kuuwa watu wasiopungua 25. Mlipuko mwingine ulitokea karibu na kanisa katika mji wa Jos kaskazini-mashariki ya nchi hiyo.

Mashambulizi hayo ya Jumapili yanaonyesha nia ya kundi la Boko Haram kuendeleza vitendo vyake vya kigaidi nchini humo huku likiwa limeuwa watu wasiopungua 491 mwaka huu, kulingana na idadi ya shirika la habari la Associated Press.

Baada ya mabomu hayo msemaji wa Boko Haram aliyetumia jina la Abul-Qaka alidai kuwa kundi hilo ndio lililofanya mashambulizi hayo katika mahojiano na gazeti moja la The Daily Trust ambalo linasomwa zaidi katika eneo la kaskazini kwenye waislamu wengi

XS
SM
MD
LG