Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 03:52

Boko Haram laanza kuteka nyara wanawake na watoto


Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau (katikati), akiwa na wanachama wengine 6. Mar. 5, 2013.

Kundi lenye siasa kali la Boko Haram lasema limeanza kuteka nyara wanawake na watoto kupinga serikali ya Nigeria.

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu nchini Nigeria, Boko Haram limesema limeanza kuteka nyara wanawake na watoto kama sehemu ya kampeni yake kuipinga serikali.

Kiongozi mchochezi wa kundi hilo Abubakar Shekau alitoa maelezo hayo katika mkanda wa video Jumatatu. Video hiyo inaonyesha kundi la wanawake na watoto wakiwa wameshikiliwa mateka lakini halikuwatambulisha.

Katika mkanda wa video Shekau pia alidai kuhusika na mashambulizi kaskazini
mashariki mwa Nigeria kwenye mji wa Bama na Baga. Hata hivyo kiongozi huyo wa wanamgambo alisema jeshi la Nigeria lilihusika na vifo vingi katika ghasia za Baga ambako takriban watu 200 waliuwawa.

Wakazi katika eneo hilo wanawalaumu wanajeshi kwa kusababisha vifo vingi kwa kuwasha mioto ,tuhuma ambazo jeshi limekanusha.
XS
SM
MD
LG