Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 00:24

Boko Haram yatoa video ya wasichana waliotekwa 2014


Boko Haram imetoa video ikionesha wasichana waliowateka 2014 huko Nigeria.
Boko Haram imetoa video ikionesha wasichana waliowateka 2014 huko Nigeria.

Serikali ya Nigeria inasema inawasiliana na kundi la Boko Haram baada ya video mpya kutolewa kwenye mtandao jana jumapili ikionesha takribani wanafunzi wasichana 50 wa Chibok waliotekwa mwaka 2014.

Kundi hilo la wanamgambo linasema wasichana kadhaa wamefariki na wanataka mabadilishano ya mfungwa kwa wasichana waliobakia. Video hiyo ya dakika 11 iliyobandikwa kwenye mtandao wa You Tube siku ya Jumapili inamuonesha mwanamme mmoja aliyejifunika uso na kuvalia nguo za jeshi akiwa na darzeni ya wasichana waliovaa hijab wakiwa pembeni yake baadhi wakiwa wamekaa chini.

Katika lugha ya kihausa mwanamme huyo katika kanda ya video anaitaka serikali ya Nigeria kuwaachia watu ambao wamewashikilia huko Abuja, Lagos na Maiduguri. Ni madai ambayo kundi la Boko haram imewahi kuyatoa awali, wanaharakati wanasema ili kuwanusuru wasichana wa Chibok wakati umefika kwa serikali ya Nigeria kufanya mashauriano.

XS
SM
MD
LG