Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:45

Blinken akutana na Rais wa Misri Alhamisi wakati akikaribia kukamilisha ziara ya Mashariki ya Kati


Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, (Kulia) akiwa na waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, mjini Cairo. January 11, 2024.
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, (Kulia) akiwa na waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, mjini Cairo. January 11, 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Alhamisi anakutana na rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi, wakati kukiwa na juhudi za kudhidbi vita vya Israel na Hamas huko  Ukanda wa Gaza, pamoja na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo huko Gaza.

Misri imekuwa na jukumu kuu katika mashauriano ya awali yaliyopelekea sitisho la muda la mapigano, wakati ambapo Hamas, iliwaachilia zaidi ya mateka 100, huku Israel ikiachilia zaidi ya wafungwa 240 wa kipalestina.

Jenerali mstaafu wa jeshi Frank McKenzie, aliyewahi kuwa kamanda wa kikosi cha kamandi kuu ya Marekani, Jumatano katika mahojiano kwa njia ya Webinar, alielezea wasi wasi wake kuhusu kuachiliwa kwa mateka waliobaki mikononi mwa Hamas.

Mazungumzo ya Blinken mjini Cairo yanafanyika siku moja baada ya kukutana na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, huko Ukingo wa Magharibi, wakati pia Abbas baadaye akikutana na Al Sissi pamoja na mfalme wa Abdullah wa Jordan.

Forum

XS
SM
MD
LG