Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 09:47

Blatter kujiuzulu urais FIFA


Rais wa FIFA Sepp Blatter akihutubia waandishi wa habari mjini Zurich, Switzerland, Juni 2, 2015.
Rais wa FIFA Sepp Blatter akihutubia waandishi wa habari mjini Zurich, Switzerland, Juni 2, 2015.

Rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA, Sepp Blatter, atajiuzulu uongozi wa shirikisho hilo kufuatia kashfa ya rushwa inayokabili baadhi ya maafisa wake na ameahidi kuitisha uchaguzi mpya karibuni kuchagua kiongozi mpya.

Blatter mwenye umri wa miaka 79 alichaguliwa tena kushika awamu ya tano Ijumaa, May 29, siku mbili baada ya kulipuka kwa habari za mgogoro wa rushwa na kukamatwa kwa maafisa saba wa shirikisho hilo mjini Zurich kabla ya mkutano mkuu wa FIFA.

"Utawala huu hauelekewi kuungwa mkono na kila mtu katika ulimwengu wa kandanda," alisema Blatter katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa haraka haraka jumanne.

Uchaguzi wa kupata mtu atakayechukua uongozi wa shirikisho hilo utafanyika kati ya Disemba mwaka huu na March mwakani.

"Nitaendelea kufanya kazi zangu (mpaka uchaguzi mpya utakapofanyika)," alisema Blatter.

Siku tatu zilizopita, Blatter alionyesha ukaidi akijibu maswali ya waandishi wa habari na kusema kamwe hatajiuzulu uongozi wa FIFA. Sepp Blatter alijiunga na FIFA mwaka 1975 kama mkurugenzi wa ufundi na miradi ya maendeleo ya soka, alipanda cheo kuwa katibu mkuu mwaka 1981 na kwa miaka 17 alikuwa msaidizi mkuu wa rais wa siku nyingi wa FIFA Joao Havalange wa Brazil kabla ya kuchaguliwa kuongoza shirikisho hilo.

XS
SM
MD
LG