Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:40

Rais wa Cameroon, Paul Biya aadhimisha miaka 39 madarakani


Wafuasi wa Rais Paul Biya wamekutana huko Monatele November 6, 2021.
Wafuasi wa Rais Paul Biya wamekutana huko Monatele November 6, 2021.

Wafuasi wa kiongozi wa pili kwa kuwepo madarakani kwa mrefu barani Afrika, Rais Paul Biya wa Cameroon mwenye umri wa miaka 88 walisherehekea kuwepo kwake katika uongozi kwa miaka 39 siku ya Jumamosi. Biya, ambaye amekuwa rais wa Cameroon tangu mwaka 1982, ni nadra sana kuonekana hadharani.

Wafuasi wa chama tawala cha Cameroon, Cameroon Peoples’ Democratic Movement, CPDM, wamekuwa wakisherehekea uongozi wa Rais Paul Biya na kusema anaweza bado kutawala taifa hilo la Afrika ya Kati kwa miaka mingine saba kuanzia mwaka 2025.

Biya alitangazwa mshindi katika uchaguzi wa mwaka 2018 akiwa amepata zaidi asilimia 80 ya kura.

Mijini na vijijini kote nchini Cameroon watu walikuwa wakiimba kushrehekea uongozi wa miaka 39 wa Biya.

Tukio moja lilifanyika Monatele, mji mkuu wa Lekie, idara iliyo karibu na mji mkuu wa Cameroon, Yaounde. Henri Eyebe Ayissi, Waziri mali za taifa, utafiti na milki ya ardhi , na mashirika wa karibu wa Biya aliongoza ujumbe wa chama cha CPDM kwenda Lekie na kuwasilisha kile alichokiita ni ujumbe maalum wa mfuasi wa Biya.

Ayissi anasema CPDM anaomba yawepo maridhiano ya kiataifa kwa Biya kuwania awamu mpya ya uongoz mwaka 2025. Anasema huko Lekie wanamuomba Biya akubali wito wa kuwania tena urais mwaka 2024 na kuendeleza kazi nzuri anayoifanya nchini Cameroon.

“Biya ameendeleza umoja licha ya ugaidi wa Boko Haram kwenye upande wa kaskazini mwa Cameroon kwenye mpaka na Nigeria na mzozo wa wale wanaotaka kujitenga ambao umesababisha vifo vya takriban watu 3,000 katika mikoa inayotumia lugha ya kiingereza,” amesema Ayissi.

Ayissi amesema mamilioni ya watoto nchini Cameroon wana fursa ya elimu kwasababu Biya amejenga shule na vyuo vikuu katika mijiji na vijiji kadhaa katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Wito wa Biya kuwania tena urais wakati muhula wake wa sasa wa miaka saba unamalizika mwaka 2025 umeungwa mkono katika miji kadhaa na vijiji mbali mbali, na kuchochea ukosoaji mkubwa kutoka kwa wapinzani wa Biya.

Christopher Ndong ni katibu mkuu wa Cameroon Renaissance Movement – chama ambacho kinadai kuwa mgombea wake, Maurice Kamto, alishinda uchaguzi wa mwaka 2018 na kwamba Biya aliiba ushindi wake. Ndong anasema. Kumtaka Biya kuwania tena uongozi mwaka 2025 kuna maana kuwa CPDM inataka kiongozi huyo afie madarakani.

“Ni kudharau wacameroon abn demokrasia ya nchi hii. Kutokana na umri wake, atafanya nini akipewa tena madaraka? Hivi sasa, hajishughulishi. Kwa kweli, huu ni uchochezi kwa utaratibu. Angalia vurugu zote ambazo zinatokea. Nchi ina madeni. Kwa kweli, inaonyesha kwamba hakuna mtu katika uongozi. Wito wa mwaka 2025 usitiliwe maanani kwasababu tunafahamu kuwa hali na afya ya mkuu wa nchi haitamruhusu kutawala nchi hii mwaka 2025.”

Ngole Ngole Elvis, mkuu wa chuo cha chama cha CPDM na mshauri wa karibu wa Biya, anasema wito kwa Biya kuwania tena ni wa kidemokrasia. Anasema badala ya kulalamika kwamba Biya amekuwepo madarakani kwa muda mrefu, upinzani ni vyema ujitayarishe kwa upigaji kura wa kidemokrasia badala ya kusema wanadhani nani anafanaa kuwaniauraisia mwaka 2025.

“Wasubiri uchaguzi ujao na kuhakikisha kwamba wamejitayarisha kwa njai ambayo itakuwa ya uhuru, ni vyema wajiandae kwa mikakati sahihi ya kampeni, ujumbe sahihi wa kampeni, ilani inayofaa, na wagombea wanaofaa,” amesema Elvis.

Biya alihudumu kama waziri mkuu kwa miaka sabab kabla ya kuwa rais. Mwaka 2008, aliondoa katika katiba viwango vya rais kuhudumu, na kumruhusu kuwania kwa kipindi kisichokuwa na kikomo.

Hivi sasa ni kiongozi wa pili kwa kuhudumu kwa muda mrefu madarakani barani Afrika chini ya jangwa la Sahara, wa kwanza ni jirani yake Rais wa Equatorial Guinea Theodoro Obiang Nguema ambaye ameshikilia madaraka tangu mwaka 1979.

XS
SM
MD
LG