Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 06:59

Birmingham ilikuwa kitovu cha ubaguzi wa rangi Marekani.


March On Washington Photo Gallery
Miongo mitano iliyopita Dr.Martin Luther King jr, alipigania usawa wa rangi kusini mwa Marekani. Hali ya nchi ilikuwa tofauti sana wakati wamarekani weusi walikuwa wakinyimwa haki za msingi za binadamu kwasababu ya sheria za mji na jimbo zilizokuwa na ubaguzi zilizowekwa kuwatenganisha watu weusi na weupe.

Birmingham ilikuwa ni eneo lililojulikana kwa ubaguzi wa hali ya juu huko Kusini, mfano ulikuwa hapo Lyric Theatre. Wateja wazungu waliingia kupitia mlango wa mbele na wakati weusi ilibidi wapitie kwenye kichochoro kwa nyuma ili waweze kuingia katika mlango ulioandikwa weusi tu.

Jamii nyingi za kusini zilipitisha sheria za kutenganisha weusi na weupe kwenye migahawa, shuleni na maeneo mengine ya umma. Mbunge John Lewis ambaye amekulia Alabama vijijini anasema ameonja matunda machungu ya ubaguzi.
Mwanaharakati wa haki za kiraia Hollis Watkins kutoka Mississippi anakumbuka baadhi ya sheria ambazo si za maandishi . Kati ya watu weupe wa kusini kulikuwa na upinzani mkali katika kubadili maisha huko kusini.

Mwezi Juni 1963 Gavana wa Alabama George Wallace aliwazuia watu wawili weusi kujiunga na chuo kikuu cha Alabama ambacho kilikuwa cha weupe peke yake. Baada ya wakuu wa usalama na jeshi la taifa kuingilia kati Wallace akasogea pembeni. Kwa mtoto wake Peggy ilikuwa ni kumbu kumbu mbaya sana.

Iliitia dosari Alabama lakini pia imemtia dosari George Wallace kwa maisha yake yote na hata alipobadilika katika miaka ya baadaye kuhusu masuala ya ubaguzi wa rangi.

Alama za ubaguzi wa rangi zilianza kupotea kusini baada ya kupitishwa kwa sheria ya haki za kiraia mwaka 1964 na kuwapa mamilioni ya wamarekani weusi uhuru na ukombozi, ambao ulifurahiwa na watu wengine katika nchi ambayo ilikuwa na watu weupe wengi.
XS
SM
MD
LG