Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 23:57

Biden kutowania urais Marekani


Makamu rais wa Marekani Joe Biden
Makamu rais wa Marekani Joe Biden

Makamu rais wa Marekani Joe Biden atangaza rasmi kuwa hataingia katika kinyang’anyiro cha ugombea urais kwa chama cha Democrat. Biden alitangaza hayo katika Rose Garden, White House, mjini Washington akiwa amezungukwa kwa Rais Barack Obama na bibi Biden, Jill.

Tangazo hilo la Biden limekuwa likisubiriwa kwa hamu katika wiki za hivi karibuni huku kinyang'anyiro cha ugombea urais kwa chama cha Democrat kikiwa kimeshikiliwa na Waziri wa mambo ya nje wa zamani Hillary Clinton.

Uamuzi wa Biden kutowania ugombea bila shaka utamwongezea nguvu Bibi Clinton ambaye ilitazamiwa kuwa ushindani wake wa kweli katika chama hicho ungeweza kutoka tu kwa Biden. Sasa Clinton atakuwa anapambana na mshindani wake wa karibu Bernie Sanders pekee.

Biden asema “ingawa sitakuwa mgombea lakini sitakaa kimya” nitaendelea kuzungumzia maswala yanayohusu watu wa tabaka la kati.

XS
SM
MD
LG