Wakati mashambulizi ya Russia yakiendelea nchini humo, Biden ataadhimisha mwaka mmoja wa vita hivyo kwa hotuba katika nchi jirani ya Poland Jumanne, amesema msemaji wa baraza la usalama wa taifa, John Kirby.
White House imesema hakuna mipango kwa Biden kuitembelea Ukraine wala kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakati wa ziara yake, lakini wachambuizi wanasema kuna dalili wawili hao wanaweza kukutana Poland. Viongozi hao wawili walikutana mwishoni mwa Desemba wakati Zelenskyy alipofanya ziara ya kushutukiza Washington DC.
Wadadisi wanasema Moscow inaugeuza mzozo huo kuwa ni vita vya kushtukiza katika juhudi ya kuzima azma ya wa Ukraine na kuuchosha ustahmilivu wa Magharibi.Ukraine imekuwa na fursa nzuri ya kupata silaha za hali ya juu kutoka Magharibi, lakini Russia inanufaika kutoka ka ukubwa wa uchumi wake, wafanyakazi na uwezo wa kiulinzi.