Rais da Silva, alichukua hatamu za uongozi mapema mwezi Januari baada ya kumshinda kwa idadi ndogo ya kura rais wa zamani wa mrengo mkali wa kulia, Jair Bolsonaro, katika uchaguzi wa marudio wa mwezi Oktoba.
Wiki moja baada ya kuapishwa, maelfu ya wafuasi wa Bolsonaro walivamia mji mkuu na kuharibu majengo muhimu ya serikali, wakiomba uchaguzi wa Lula ubatilishwe.
Biden alilaani kitendo hicho na aliahidi msaada wa Marekani.
Wachambuzi wanasema ziara hiyo ni muhimu kwa Lula kupata uungaji mkono wa Marekani kusaidia kuuonyesha ulimwengu kwamba taifa lake lina uthabiti wa kisiasa.
Katika taarifa, White House imesema Biden na Lula watajadili jinsi nchi hizo mbili zinaweza kuendelea kushirikiana ili kudumisha ushirikishwaji na maadili ya kidemokrasia katika kanda hiyo na ulimwenguni kote, hasa kabla ya mkutano kuhusu Demokrasia wa Machi 2023.
Facebook Forum