Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:56

Biden kukutana na rais wa Ufilipino wakati mgogoro na China ukiendelea


Rais wa Marekani Joe Biden April 29, 2023 Picha: Reuters
Rais wa Marekani Joe Biden April 29, 2023 Picha: Reuters

Rais wa Marekani Joe Biden atakutana na mwenzake wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr katika ikulu ya White House leo Jumatatu wakati hali ya wasiwasi ikiwa inaongezeka kuhusiana na jeshi la majini la China, kuendelea kusumbua meli za Ufilipino katika bahari ya South China.

Marcos anatembelea Washington baada ya Marekani na Ufilipino kumaliza mazoezi makubwa ya kijeshi kuwahi kuandaliwa na nchi hizo mbili.

Ziara hiyo pia inafanyika wakati wanajeshi wa angani wa Marekani na Ufilipino wanafanya mafunzo ya kutumia ndege za kivita nchini Ufilipino, ambayo ni ya kwanza kufanyika tangu mwaka 1990.

Ufilipino ulikubali kutoa nafasi 4 kwa jeshi la Marekani kuweka kambi zake kwenye kisiwa hicho, wakati Marekani inatafuta njia za kuzuia China kuendelea na vitendo vyake vya uchokozi dhidi ya Taiwan katika bahari ya South China Sea.

Wakati huo huo, China inaripotiwa kuikasirisha Ufilipino kwa kuendelea kusumbua meli za kivita na walinzi wa pwani wa Ufilipino, pamoja na kuwafukuza wavuvi wa Ufilipino walio kwenye mipaka ya Ufilipino, ambayo Beijing inadai kumiliki.

XS
SM
MD
LG