Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:50

Biden kukutana na Macro kwa mazungumo ya kibiashara na usalama


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) na mke wake Brigitte Macron wakishuka ndege baada ya kuwasili Maryland, Marekani Nov 29
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) na mke wake Brigitte Macron wakishuka ndege baada ya kuwasili Maryland, Marekani Nov 29

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macro anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden hapa Washington DC kujadiliana maswala kadhaa yakiwemo ya kusawazisha sera za Marekani na Ufaransa kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine, na namna ya kurahihisha biashara.

Macron anakuwa rais wa kwanza kupata mwaliko wa kitaifa mara mbili, mara ya kwanza ikiwa mwaka 2018 wakati wa utawala wa Donald Trump, amapo alitolewa heshima kwa kufyatuliwa mizinga 21.

Ataandamana na mawaziri na wanadiplomasia kadhaa, pamoja na viongozi wa kibiashara.

Maafisa wa serikali ya Ufaransa wamesema kwamba kuna maswala muhimu ambayo Marekani inaweza kushirikiana na Ufaransa.

Ushirikiano kati ya Marekani na Ufaransa umepungua kwa mwaka mmoja sasa, tangu Marekani ilipopata mkataba wa gharama kubwa, wa uuzaji wa nyambizi kwa Australia na kuanzisha ushirikiano na Uingereza katika bahari ya Pacific.

XS
SM
MD
LG