Changamoto hizo ni pamoja na vita vya Ukraine, mabadiliko ya hali ya hewa, biashara, uhamiaji na ushawishi wa China. Kwa mijibu wa shirika la habari la AP makubaliano mawili muhimu yalionekana kuwa kwenye ajenda hata kabla ya Biden kuondoka Washington.
Canada itaongeza muda wake wa uimarishaji wa kijeshi kwenye kamandi ya Ulinzi wa Anga ya Kaksazini mwa Marekani, wakati mataifa yote mawili yakiwa tayari yamefikia makubaliano ya kufanya marekebisho kwenye sheria za uhamiaji kwa watu wanotafuta hifadhi, kulingana na maafisa wa Canada na Marekani.
Hata hivyo maafisa hao hawakutoa taarifa za kina kuhusu masuala hayo.Kama sehemu ya makubaliano hayo, Canada inatarajiwa kutangaza kwamba wahamiaji 15,000 kutoka Ukanda kwa Kaskazini watapewa nafasi ya kuomba hifadhi kuingia nchini humo, kulingana na afisa wa Canada.
Ikulu ya Marekani haikutoa taarifa zozote kuhusu makubaliano hayo yanayotarajiwa kutangazwa rasmi Ijumaa. Ziara hiyo imefanyika wakati utawala wa Biden ukiweka kipaumbele cha kuimarisha uhusiano na Canada katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.