Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 12:21

Biden atembelea Puerto Rico baada ya kimbunga


Rais Joe Biden na mke wake Jill wakielekea kwenye ndege kuelekea Puerto Rico
Rais Joe Biden na mke wake Jill wakielekea kwenye ndege kuelekea Puerto Rico

Rais wa Marekani Joe Biden pamoja na mke wake Jill Biden, Jumatatu wamesafiri Puerto Rico ili kujionea  juhudi  zinazoendelea katika kurejesha hali ya kawaida, baada ya  kimbunga Fiona kukipiga kisiwa hicho kinachomilikiwa na Marekani mwezi uliopita.

White House imesema kwamba Biden atazungumzia azma ya utawala wake ya kuwasaidia wakazi wa Puerto Rico katika kujenga miundombinu inayoweza kustahimili majanga. Taarifa hiyo imeongeza kwamba Biden atatangaza msaada wa dola milioni 60 za ujenzi wa kuta za kuzuia mafuriko pamoja na kuunda mifumo ya kisasa ya kuonya kuhusu vimbunga.

Biden pia atakutana na familia zilizoathiriwa , viongozi wa kijamii pamoja na timu za uokozi. Gavana wa Puerto Rico Pedro Pierluisi amesema kwamba serikali yake pamoja na timu za uokozi watatumia nafasi hiyo kumueleza Biden moja kwa moja kuhusiana na hali halisi. Kampuni ya kusambaza umeme kisiwani humo ya LUMA imesema Jumapili kwamba imerejesha huduma hiyo kwa takriban asilimia 92 ya wakazi.

XS
SM
MD
LG