Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 03:13

Biden apongeza makubaliano ya vyama vya wafanyakazi wa reli na waajiri


U.S. President Biden hails U.S. railway labor agreement following talks in Washington

Rais wa Marekani Joe Biden alisema mapema Alhamisi vyama vya wafanyakazi wa huduma ya reli na waajiri wake vimefikia makubaliano ya muda kuhusu malipo bora na kuboresha hali ya mazingira ya kazi kwa ajili ya kuepusha mgomo wa huduma za reli nchi nzima.

“Huu ni ushindi kwa maelfu ya wafanyakazi wa reli ambao wamefanya kazi kwa bidii katika kipindi cha janga la COVID-19 kuhakikisha familia za Marekani na jamii zake wanapata mizigo yao kitu kilichofanya sisi kuendelea na maisha wakati wa miaka hii migumu,” Biden alisema.

Waziri wa Kazi Marty Walsh alituma ujumbe wa tweet kuwa makubaliano hayo yamefikiwa baada ya masaa 20 ya mazungumzo kati ya kampuni za reli na vyama vya wafanyakazi.

Marty Walsh
Marty Walsh

Walsh alisema makubaliano hayo “yameleta uwiano kati ya mahitaji ya wafanyakazi, biashara na uchumi wa taifa letu.”

“Mfumo wa reli yetu ni muhimu kwa mnyororo wa usambazaji, na iwapo kungetokea mgomo ungekuwa na madhara kwa viwanda, wasafiri and familia nchi nzima,” Walsh alisema..

Mabehewa ya treni yakiwa huko katika yadi iliyoko kusini mwa Norfolk, Atlanta, Georgia, Sept. 14, 2022.
Mabehewa ya treni yakiwa huko katika yadi iliyoko kusini mwa Norfolk, Atlanta, Georgia, Sept. 14, 2022.

Vyama vya wafanyakazi vimekuwa vinataka ongezeko la mshahara na mazingira bora ya kazi, pamoja na mabadiliko ya sera za mahudhurio ambazo wafanyakazi walisema inawia ugumu kwa kuchukua likizo kwa ajili ya kumuona daktari.

Wanachama wa vyama vya wafanyakazi lazima waidhinishe makubaliano haya ya muda.

Biden ameyaita makubaliano haya “ni ushindi muhimu kwa uchumi wetu na watu wa Marekani.”

“Wafanyakazi hawa wa shirika la reli watapata malipo bora, mazingira ya kazi yataboreshwa, na kutakuwa na utulivu wa moyo juu ya gharama za malipo ya huduma ya afya zao: zote hizo zimefikiwa kwa tabu," Biden alisema katika taarifa yake.

“Makubaliano hayo pia ni ushindi kwa makampuni ya reli ambayo yataweza kuendelea kuwaajiri wafanyakazi hao na kuajiri zaidi kwa ajili ya huduma ambayo itaendelea kuwa ni ute wa mgongo wa uchumi wa Marekani kwa miongo mingi ijayo.

Mgomo uliyokuwa unaelekea kuwepo ulileta hofu kwa kuzorota kwa usafirishaji wa mizigo muhimu nchi nzima.

Some information for this report came from Reuters and The Associated Press.

Baadhi ya taarifa katika repoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya Reuters na AP

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG