Marekebisho hayo yanashinikizwa na serikali ya mrengo mkali wa kulia ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu, na ambayo yamepelekea maandamano ya kitaifa.
Bunge la Israel Jumatatu linaanza mchakato wa marekebisho hayo ambayo yanalenga kuongeza serikali nguvu katika kuchagua majaji, huku nguvu za mahakama ya juu zikipunguzwa au kanuni dhidi ya utawala.
Mchakato huo umezua maandamanao ya kitaifa wakati kukiwa na wito wa mashauriano zaidi, huku kura ya maoni ikionyesha uunganji mkono mdogo kutoka kwa raia.
Gazeti la The New York Times limemnukuu Biden akisema kwamba ”Demokarsia za Marekani na Israel zimejikita kwenye misingi ya taasisi zenye nguvu kwenye usimamizi na uangalizi wa kuwa na mahakama huru.” Ameongeza kusema kwamba ni muhimu kuwahusisha watu wote, ili kupata marekebisho yatakayokuwa endelevu.
Facebook Forum