Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 15:54

Biden anaangalia kufadhili upanuzi wa huduma ya uzazi wa mpango wa dharura


USA-BIDEN/
USA-BIDEN/

Amesema hilo ndio jibu linalowezekana ikiwa mahakama ya juu itabatilisha uamuzi wa mwaka 1973 ambao ulihalalisha utoaji wa mimba nchini kote.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki amesema utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden unaangalia msaada wa fedha kusaidia kupanua ufikiaji wa huduma ya uzazi wa mpango wa dharura.

Amesema hilo ndio jibu linalowezekana ikiwa mahakama ya juu itabatilisha uamuzi wa mwaka 1973 ambao ulihalalisha utoaji wa mimba nchini kote.

Psaki msemaji wa ikulu ya Marekani Psaki ameeleza kuwa:" Kitu tunachozingatia sana ni athari gani itakuwepo. Ingepunguza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma za uzazi hasa kwa wanawake wenye kipato cha chini wanawake wa rangi tofauti, wanawake walioko vijijini. Tunajua kwamba asilimia 75 ya wale wanaotaka kutoa mimba wanaishi chini ya asilimia 200 ya kiwango cha umasikini. Na wagonjwa wengi wanaotaka kutoa mimba hujitambulisha kama weusi, wa Spanish, na AAPI.

Ameendelea kusema: Kwa hiyo ukiangalia majimbo 26 tuchukue kwa mfano, 13 hadi 26, kutegemeana na ramani hiyo inamaanisha kuwa wanawake ambao wengi wao wako chini ya kiwango hicho cha umasikini ni Weusi , wa Spanish, au AAPI. Watalazimika kufikiria jinsi ya kusafiri, jinsi ya kuchukua muda wa mapumziko kazini, jinsi ya kupata huduma ya watoto. Ni gharama kubwa. Haitakuwa salama na hilo ndilo tunalolenga kufanyia kazi kushughulikia tunapofanya maamuzi ya kisera na kuzingatia. “

XS
SM
MD
LG