Wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil mwenye msimamo wa mrengo mkali wa kulia Jair Bolsonaro Jumapili walivamia majengo ya Bunge, Ikulu na Mahakama ya Juu, ikikumbusha shambulio la Januari 6 mwaka 2021 kwenye Bunge la Marekani lililotekelezwa na wafuasi wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Mamlaka za Brazil zimewakamata zaidi ya wafuasi 1,000 wa Bolsonaro kufuatia uvamizi huo wa Jumapili.