Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:51

Biden amerudia nia yake ya kutuma hundi kwa mamilioni ya wamarekani


Rais wa Marekani, Joe Biden akizungumza akiwa White House, Jan. 27, 2021.
Rais wa Marekani, Joe Biden akizungumza akiwa White House, Jan. 27, 2021.

Rais Biden anatoa wito wa kupitishwa haraka pendekezo lake la mfuko wa auheni ya msaada wa dola trilioni 1.9 za virusi vya Corona unaojumuisha hundi huku akiweka kando wito uliotolewa na maseneta wa Republican kwa mpango mdogo zaidi wa dola bilioni 618

Rais wa Marekani Joe Biden amerudia tena nia yake ya kutuma msaada wa dola 1,400 kwa mamilioni ya wamarekani watu wazima ili kuinua uchumi wa nchi ulioharibika kutokana na janga la virusi vya Corona. Lakini anasema anakaribisha maoni kufuatia madai ya waRepublican kuongeza masharti juu ya nani atapata fedha hizo.

Akitoa hotuba kwa wabunge wa Democratic katika baraza la wawakilishi na baadae kwenye mkutano wa kundi la maseneta wa Democratic, Rais Biden alitoa wito wa kupitishwa haraka pendekezo lake la mfuko wa auheni ya msaada wa dola trilioni 1.9 za virusi vya Corona ambao unajumuisha hundi huku akiweka kando wito uliotolewa na baadhi ya maseneta wa Republican kwa mpango mdogo zaidi wa dola bilioni 618.

Rais Biden amewaambia wabunge kwamba yupo tayari kuweka kikomo cha mapato ya chini juu ya nani atapata hundi za dola 1,400 lakini sio kupunguza ukubwa wa malipo.

Sambamba na malipo ya dola 600 yaliyoidhinishwa na Rais wa zamani Donald Trump mwezi Disemba mwaka jana, msaada wa dola 2,000 kwa pamoja utakuwa sawa na ahadi ya Biden aliyotoa wakati wa kampeni yake ya ushindi kwa White House mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG