Pamoja na mke wa Rais, Jill Biden, waathirika, wanafamilia, na watetezi wa ugonjwa huo walikusanyika kukumbuka wale wote waliopoteza maisha ya ugonjwa huo. Rais Biden, alisisitiza serekali kuu inasaidia watu milioni 1.2 ndani ya Marekani, wanaoishi na VVU ambavyo vinasababisha UKIMWI.
Kulikuwa na kitambaa chenye sehemu 124 za kukumbuka watu waliofariki dunia kutokana na magonjwa yanayo husiana ya UKIMWI.
Mpaka sasa kuna watu milioni 40 duniani kote wanaoishi ya VVU, kwa mujibu wa White House.
Utawala wa Rais Biden, imefanya uwekezaji kadhaa wa kuzuia ugonjwa guo, na kuondoa unyanyapaa unaowakabili watu wanaoishi na VVU.
Forum