Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 21:41

Beyonce' na Kelly Rolland wanasaidia kujenga nyumba Texas kwa wasio na makaazi


Beyonce Knowles (L), Michelle Williams (C) na Kelly Rowland
Beyonce Knowles (L), Michelle Williams (C) na Kelly Rowland

Mradi wa nyumba wa Knowles-Rowland wenye thamani ya dola milioni 8.4 katika mji wa Houston kwenye jimbo la Texas nchini Marekani utaanza mwezi Oktoba

Wasanii maarufu nchini Marekani, Beyoncé Knowles na Kelly Rowland wanaonyesha juhudi zao za pamoja kuzisaidia jamii katika jimbo la Texas kwa kuwajengea nyumba, kituo cha afya ya akili na mahitaji mengine ya kibinadamu.

Mradi wa nyumba wa Knowles-Rowland wenye thamani ya dola milioni 8.4 utaanza mwezi Oktoba. Wakati huo huo mradi wa American Rescue Plan unachangia dola milioni 7.2 katika mradi huo na fedha za ziada zinatoka kwa vikundi vya nje, ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Rice. Eneo hilo litakuwa na nyumba mpya 31 za makazi ya kudumu na litakuwa pia na mameneja wa ustawi wa jamii, watoa ushauri kwa vijana, huduma ya msaada katika usafiri, huduma ya afya ya akili na masuala mengineyo ya msaada wa kibinadamu.

Santa Chacha, mchambuzi wa masuala ya Burudani na kijamii kutoka Jimbo la maryland nchini Marekani anaelezea hatua hii inatoa funzo kwa wasanii wengine Marekani na Afrika kwa ujumla. Anasema ni vyema unapokuwa na uwezo kusaidia wengine.

Santa Chacha, mchambuzi wa masuala ya Burudani na kijamii.m4a
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:57 0:00

Jaji wa Kaunti ya Harris huko Texas, Lina Hidalgo alisema “Kaunti ya Harris na mji wa Houston kwa pamoja na muungano wa wasio na makazi wamepunguza idadi ya wasio na makazi katikati ya janga hilo kwa asilimia 20." Aliongeza kusema kuwa "Tulifanya tena hesabu ya watu wasio na makazi, kwa hivyo ni mipango kama hii hakika nitaiunga mkono bila kujali ni nani aliye nyuma yake, lakini ni ya kuvutia sana, nadhani, kwa sababu kuna majina haya ya Beyonce na Kelly Rowland, ambao, bila shaka, wamekuwa wakiiunga mkono jamii kwa muda mrefu sana."

Hii si mara ya kwanza kwa wanachama wa kikundi cha Destiny's Child kutoa msaada kwa mji wao. Knowles alirudi Houston kusaidia kutoa chakula kwa wale walioathirika na kimbunga Harvey mwaka 2017.

Forum

XS
SM
MD
LG