Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 00:23

Beyonce aongoza miongoni mwa wasanii waloteuliwa kwa tuzo za Grammys 2023


Beyonce akitumbiuza kwenye tamasha la Get Out the Vote mjini Cleveland Nov 4, 2016 .

Tangazo la walioteuliwa kuwania tuzo za Grammy mwaka huu limetolewa Jumanne Novemba 15, na linaonekana kuwaweka tena katika jukwaa kwa ushindani kati ya waimbaji Adele na Beyonce kuwania tena nafasi ya juu, katika sehemu mbili tofauti za mashindano hayo kama ilivyokuwa hapo mwaka 2017.

Muimbaji mashuhuri wa Marekani, Beyonce, anaongoza katika orodha ya wateule wa nishani za Grammys, akipata teuzi 9 za dhahabu, akiwa anaongoza, na Kendric Lamar, akiapta teuzi 8 nae muimbaji Adele kutoka Uingereza akipata teuzi 7 kadhalika muimbaji Brandi Carlile, ambaye nae pia amepata teuzi 7.

Tangazo la wateuzi wa mwaka huu wa Grammys limetolewa Nov 15, 2022, na linaonekana kuweka tena stegi, waimbaji Adele na Beyonce kunangania tena nafasi ya juu, katika sehemu mbili tofauti za mashindano hayo kama ilivyokuwa hapo mwaka 2017.

Baadhi ya wale waloteuliwa kunangania tuzo la albumu ya mwaka ni pamoja na Kendric Lamar, Adele, Brandi Carlile, Lizzo, Bad Bunny, Mary J Blige, HarryStyles, Abba, Coldplay na Beyonce. Utambuzi na uteule wa Beyonce unafwatia kutowa kwa albamu yake kabambe yenye miondoko ya disco ijulikanalo kama "Renaissance". Albamu liitwalo" Mr. Morale And The Big Steppers, la Kendik Lamar, Adele nae na albamu lake 30 nae Brandi Carlile na albamu lake, In These Silent Days. Waimbaji hawa wanne kadhalika nyimbo zao zimeteuliwa katika kundi la rekodi ya mwaka. Wimbo wa Adele, Easy On Me, ulitia fora sana hapo mwaka jana.

Muimbaji Adele akishikilia Grammys zake baada ya kushinda katika kundi la "Rekodi ya mwaka kwa wimbo wake "Hello" huko Los Angeles February 12, 2017
Muimbaji Adele akishikilia Grammys zake baada ya kushinda katika kundi la "Rekodi ya mwaka kwa wimbo wake "Hello" huko Los Angeles February 12, 2017

Katika kundi la msanii mpya bora, bado haiko bayana nani ataibuka mshindi, lakini baadhi ya wale waloteuliwa ni waimbaji, Anitta, Omar Apollo, Latto, Samara Joy, Tobe Nwigwe , Molly Tuttle miongoni mwa wengine wengi.

Katika miondoko ya Rap, Dj Khaled akishirikiana na Rick Ross, Lil Wayne, Jay Z, John Legend na Fridayy wanaongoza katika kundi la album bora la Rap, na wimbo "God Did". Wengine waloteuliwa katika kundi hilo ni pamoja na Jack Harlow, Future, Pusha T na Kendrik Lamar.

Kundi la mziki bora wa Reggae, limeongozwa na Kabaka Pyramid na wimbo The Kalling, Koffee na wimbo wake Gifted, Sean Paul na wimbo wake Scorcha na Shaggy, akiwa amerudi tena kwenye mziki baada ya kupotea kwa mda, na wimbo wake, Com Fly Wid Mi.

Na katika kundi la albam bora la mziki wa kimatiafa, baadhi ya wale waloteuliwa ni pamoja na Berklee Indian ensemble, Angelique Kidjo na Ibrahim Laalouf, Masa Takumi, Anoushka Shankar na Burna Boy akiwa ameingia na albam lake Love Damini.

Tuzo za Grammays za mwaka 2023 zinatarajiwa kufanyika February 5, 2023 katika ukumbi wa Crypto.com mjini Los Angeles nchini Marekani.

Ripoti hii imetaarishwa na Aida Issa

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG