Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:12

Dkt.Kiza Besigye amtaka Museveni ajitokeze kwenye mdahalo.


Kiongozi wa upinzani Uganda Dr. Kizza Besigye
Kiongozi wa upinzani Uganda Dr. Kizza Besigye
Mgombea wa urais nchini Uganda kwa tiketi ya chama cha Forum for democratic change-FDC Dkt. Kiiza Besigye, ametoa changamoto kwa mwenzake wa chama tawala cha National resistance movement-NRM rais Yoweri Museveni, kutokwepa mdahalo wa pamoja wa wagombea wote wa urais unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa wiki ijayo.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:20 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
Hii ni baada ya rais Museveni kusema kwamba hana muda wa kutosha kuhudhuria mjadala huo kutokana na ratiba zake za kampeni akisema anahutubia mikutano minne ya kampeni kila siku.
Besigye alikuwa akihutubia umati mkubwa wa watu mashariki mwa Uganda katika mji wa Mbale akiwa kwenye uwanja mmoja mjini humo uliojaa watu kupita kiasi.
Mdahalo huo umeandaliwa na taasisi za kidini na Besigye anasema itawapa wananchi wa Uganda kuchambua mbivu na mbichi kisiasa.
XS
SM
MD
LG