Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 22:19

Kiongozi wa upinzani Uganda aachiwa kwa dhamana


Kiongozi wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye akihutubia mkutano wa hadhara tarafa ya Rubaga mjini Kampala, Uganda, Februari 14, 2011

Maafisa nchini Uganda wamemwachia huru kwa dhamana kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, takriban wiki moja baada ya kukamatwa kwake kwa kuongoza maandamano dhidi ya kupanda kwa bei za bidhaa nchini humo.

Mahakama moja katika mji wa Nakasongola leo, Jumatano imempatia dhamana Besigye kwa sharti kwamba aendeleze amani kwa miezi saba ijayo. Kiongozi huyo wa upinzani ana-apa kuendelea kuandaa maandamano. Kesi yake imepangwa kusikilizwa Mei 13.

Besigye ameongoza mamia ya wafuasi katika mifululizo ya maandamano ya kutembea kwa miguu kupinga kuongezeka kwa gharama za usafiri.

Polisi wa Uganda walimkamata kiongozi huyo kwa mara ya tatu mwezi huu, wakati alipojaribu kuongoza maandamano katika mji mkuu, Kampala. Besigye alishtakiwa kwa kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria na alipelekwa jela huko Nakasongola.

Rais Yoweri Museveni analaumu kupanda kwa bei za chakula na mafuta kunatokana na ukame na sababu nyingine za kigeni kama vile kupanda kwa bei za mafuta duniani. Serikali yake inasema haitavumilia hatua za kuandamana na aliagiza polisi kuvunja maandamano matatu ya awali.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeitaka serikali ya Uganda kuheshimu haki za raia za kuandamana kwa amani.

Besigye aliwania nafasi ya rais katika uchaguzi wa mwezi Februari, lakini alishika nafasi ya pili nyuma ya bwana Museveni. Kiongozi huyo wa upinzani ameshindwa uchaguzi mara tatu mfululizo dhidi ya Rais wa muda mrefu nchini Uganda, Yoweri Museveni.




XS
SM
MD
LG